Kuna mambo yanayoendelea sasa hivi kuhusu uchaguzi wa mwenyekiti na wanachama kuu ( kamati kuu) ya chama cha wanasheria wa Kenya.Mmoja wa wale ambao anatetea kiti cha mwenyekiti ameandaa kwa mtandao chapisho lake la uchaguzi ambako wewe na mimi twaweza kuzua utata na mengineo katika uchaguzi na sera zake.
Mimi nataka kuwa mmoja wa wale ambao wataweza kulinganisha sera zake na mwongozo unaofaa katika hiki chama.Maswala nyeti ambayo lazima yatiliwe maanani yana wengi ambao wanaoyasema..kwa mtaa,,vichochoroni na kwingineko.Wengine wana utata kuhusu jambo ambalo hawawezi kueleza kinaga ubaga lakini wana hakika kuna jambo......wakilisikia watakwambia hilo ndilo jambo!!!
Wengi wa wanasheria hapa Kenya, kama Wakenya wengi kiswahili chao ni cha hali isioridhisha na kwa hivyo wengi hawataweza kusoma nitakayoandika na kuzidi kuhimiza hapa.La muhimu ni kwamba Kiswahili lazima kitukuzwe.Wengi huongea, isipokuwa si mufi, lakini huwasiliana. Hii ni njia yangu moja tuu ya kujaribu kuleta Kiswahili katika mustali wa mbele kwa mazungumzo yetu.
Swala ambao tutangazia leo ni hili la uchaguzi unaotekelezwa kupitia sanduku la posta.Katika uchaguzi wote, la makini ni kwamba kura lazima zipigwe na kukusanywa katika njia ya kuridhisha wote.Lazima kura ifanyike hadharani!!!Jambo la kusikitisha ni kwamba wanasheria leo wanatuma kura zao kwa njia ya posta na hizi kura zinakusanywa na ofisi ya kamati ya wanasheria pia zinakaguliwa baadaye na repoti kutolewa na wakaguzi.Hili ni jambo ambalo wengi wameonelea ni la hali duni kulinganisha na vile ambavyo wanasheria wenyewe huonelea ni mwafaka katika kila uchaguzi, uwe ni wa nchi au chama chochote kile.
Swala la pili ni kwamba kila mpiga kura lazima aweke sahihi kura yake na jina lake na anwani yake.Hivi ni kumaanisha ya kwamba lazima wanachama wajulikane wakati wa kura. Hili si swala kwani lazima anayepiga kura atambulike.Jambo ni kwamba wanaongangania viti huwa na uwezo wa kujua nani aliyewapigia kura au la.Kama hili si swala basi na liwe liwalo.
Haya ndiyo maswala mawili ya kwanza.Mengine itafuata.
Waweza kuungana na wanasheria katika harakati hii kutumia anwani hiihttp://lsk2007kw.blogspot.com/
HADI KESHO..INSHALLAH..ALAMSIKI!
Subscribe to:
Posts (Atom)