Thursday, November 23, 2006

Kweli, Haki ya wachapishaji ina ukingo wake hata America?( au sana sana America?)

Kweli, Haki ya wachapishaji ina ukingo wake hata America?( au sana sana America?)
Jambo! Mawazo leo tutayaelekeza kwenye tukio katika nchi ya America ambako sheria ya rekebisho la kwanza la Katiba (First Amendment) linazuia sheria yeyote ile katika Nchi ya America ambayo inanuia kuelekeza maoni au namna au la ya yale yanayochapishwa kwa gazeti au kuandaliwa katika runinga au redio. Maswala ambayo sheria ya nchi hiyo kulingana na uamuzi wa koti kuu la katiba hayaja katazwa na rekebisho la kwanza la Katiba ni kuhusu vikwazo dhidi ya yasioridisha ya mapenzi.

Kuna mengi pia ambayo wananchi wa America hawajakubalian kuhusu umbali wa rekebisho la kwanza la Katiba.
Mwanaspoti O.J. Simpson ilisemekana kutokana na yeye mwenyewe an mawakili wake na wachapishaji wa vitabu, kwamba alikuwa an kitabi na filamu ndogo, “ If I did it” kuhusu jinsi angalivyotenda mauaji aliyoondolewa lawama na koti la uhalifu lakini akapatwa na lawama na koti la haki za kawaida, huko California. Wengi, inasemekana walipandwa ma mori sana kuhusu kitabu na filamu hii ambayo iliegezea kutotilia maanani uchungu na fedheha ya wale walioaga dunia kutukia lile tendo la maauaji katika nyumba yake O.J. Simpson.
Mwekezaji mkuu wa stesheni ya Fox News, Rupert Murdoch, alionelea ya kwamba Waamerica wengi wangepotishwa na ile filamu iliyokuwa iandaliwe katika running a yake nap engine kuuokota pesa nyingi kupitia vitambulisho.
Hili ni jambo amabalo ….katika nchi zingine pengine hata halingewezekana kwa sababu sheria za nchi hizo zinakataza filamu kama hizo. Nchi ya Uingereza ni mfano sahihi. Katika nchi hii uonyeshanaji wa filamu kama iliotangazwa ingekuwa uvunjaji wa sheria. …….Pengine walio na hamaki kuhusu maswala ya Haki ya kuchapisha waweza kuonelea kwamba hata pasipo na sheria waandishi wenyewe na wanaoandaa matangazo kwa runinga kuna yale wanayotilia maanani wakati wa kazi yao.Hili ni jambo ambalo limetajwa na wengi kuwa kikwazo kisichoeleweka na wengi kuhusu uadilifu na haki ya kuchapisha an kutangaza. Kwa kimombo, wanalitamka kama, “self-censorship” na kulingana na yale yaliotukia America wiki hii, ole… rekebisho la kwanza la Katiba!!!!
Maadili na utamaduni ya wananchi wa America yaonekana bado ni mvutano kati ya sheria wasizotaka na ambazo katiba imekataa kupitishwa na mambo ambayo wengi wao ( kama wale waliofanya filamu hii isionyeshwe) wanaonelea si mwafaka( mfano ni ule utumiaji wa picha za tukio la 9/11 na chama cha Repuplican Party katika kuomba kura za Urais). Jambo ni kwamba pengine ni afadhali kutokuwa na sheria kuliko kuwa na sheria inayowanyanyasa wananachi kwa kuhujumu haki yao ya kuelezwa ukweli. America, kuna dhihirisho kwamba kuna mengi yanayotendeka kulingana na sheria ya rekebisho la kwanza la Katiba lakini pia “ self-censorship” ni jambo lisiloweza kutupiliwa mbali kama la kupotosha.Je, ni lipi zimwi likujualo?