Hamjambo tena?!
Pole , lakini singeweza kuandika chochote kwa wakati mkubwa kwa sababu nilikuwa sina la kusema. Hi ni saa sana kuhusu mambo yanayoendelea katika nchi hii na yanavyotangazwa na vyombo vyetu vya habari na sana sana kwa redio na magazeti.
Sijui kama wengi wenyu wameghadhabihswa na matangazo ya aina fulani kama vile mkenya katika mtandao ambaye nilmesahau alivyofanya.Hii ni kwa mfano redio kama vile Classic FM asubuhi na mapema Nairobi.
Kwangu mimi haya yote ni sawa, kwani lililo la muhimu ni Wakenya wenyewe wakiweza kupata nafasi ya kujieleza kwa wengine.
Mengi yatanenwa mwaka huu.Nitaangalia katika magazeti na pia televisheni na redio na kuwaletea habari za kisheria na zingine vile zilivyoletwa.
Jukumu ni lenyu kujiandaa kukubaliana na machapisho haya.
Jana katika gazeti la Daily Nation kulikuwa na machapaisho kuhusu tukio la wiki iliyopita, ijumaa, ambako walioshtakiwa kwa mauaji ya mmoja ya familia ya Akahs huko pwani, waliachiliwa hru.
Sasa familia ya Akasha imetangazwa na gazeti kwamba, linataka uamuzi wa mahakama kuu kuhusu uadilifu wa katiba katika kesi hiyo ambako inaelewka kulikuwa na uhusiano wa Mtahini na mtahiniwa kati ya jaji wa kesi na wakili aliyewakilisha waliotiliwa shaka.
Tutafuata uamuzi wa koti wiki ijayo na kuwaletea vipi itikavyoamuliwa.
P.S. NAELEZWA KWAMBA TUKIO LA MUHIMU KUHUSU UCHAGUZI WA MKUU WA KITIVO CHA SHERIA KATIKA CHUO KIKUU CHA NAIROBI LIMETENDEKA AMBAKO MWANASHERIA DAKTARI KAMERI MBOTE AMETAWAZWA KUWA MSHINDI. IJAPOKUWA KUNA UTATANISHI KUHUSU TUKIO HILI AMBALO LAWEZA TUU KUTATULIWA NA KAMATI KUU YA CHUO HICHO.MENGI WIKI IJAYO KUHUSU JAMBO HILI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment